Numbers 26:28-37

28 aWazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:

29 bWazao wa Manase:

kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi);
kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.
30 cHawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi:
kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri;
kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki;
31kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli;
kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu;
32kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida;
kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi.
33 d(Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)
34 eHizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.

35 fHawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:

kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela;
kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri;
kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;
36Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela:
kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani.
37 gHizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500.

Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao.

Copyright information for SwhNEN